NightKept: Taarifa kwa walinzi
Kiswahili
NightKept inarekodi nini? Unapobonyeza "Start Patrol", programu ya NightKept inarekodi mahali simu yako ilipo hadi utakapomaliza doria. Inaendelea kurekodi hata simu ikiwa imefungwa au programu imefungwa. Hairekodi mahali ulipo wakati mwingine wowote.
Utajuaje inarekodi? Ujumbe "NightKept — Patrol Active" unaonekana kwenye simu yako muda wote inaporekodi.
Kwa nini? Ili mwajiri wako aone kwamba doria zilifanyika. Taarifa hizi hazitumiki kwa matangazo na haziuzwi kamwe.
Nani anaziona? Mwajiri wako pekee, na wafanyakazi wachache wa NightKept wanapohitaji kusaidia au kulinda huduma.
Zinahifadhiwa kwa muda gani? Miezi 12 baada ya doria kuisha, kisha zinafutwa. Doria iliyosahaulika inamalizika yenyewe baada ya saa 14.
Haki zako Unaweza kuomba nakala ya taarifa zako, kuzirekebisha au kuzifuta. Ni bure.
- Tembelea nightkept.ke/delete-account
- Au tuma barua pepe kwa privacy@nightkept.ke
- Au muulize mwajiri wako
Ukiwa na malalamiko, unaweza pia kuwasiliana na Ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa Data: odpc.go.ke
Maelezo kamili (kwa Kiingereza): nightkept.ke/privacy